Burudani

Sauti Sol kupanda jukwaa moja na Beyonce, Usher kwenye Global Citizen Festival

Kundi la Sauti Sol la nchini Kenya litapanda kutumbuiza kwenye jukwaa moja na wasanii wakubwa wa Marekani akiwemo Beyonce kwenye Global Citizen Festival itakayofanyika Jumamosi hii jijini New York.

Festival

Wasanii wengine watakaotumbuiza ni pamoja na Usher, Common na Tori Kelly. Kwenye tamasha hilo mastaa wengine watakaoshiriki ni muigizaji wa filamu, Leonardo DiCaprio, Bono, mshindi wa Nobel Peace Prize, Malala Yousafzai pamoja na Bill na Melinda Gates.

“SEE YOU SOON NEW YORK!! We are off to perform at the Global Citizen Festival! Other performers will include BeyoncĂ©, Ed Sheeran and Coldplay among others. The festival going down on Saturday will be broadcasted live on YouTube and NBC,” wameandika Sauti Sol kwenye Instagram.

Tamasha hilo ni sehemu ya mkutano wa viongozi wakuu wa mataifa mbalimbali kwenye umoja wa mataifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ban Ki-Moon naye atakuwepo.

Washereheshaji watakuwa pamoja na Stephen Colbert, Kerry Washington, Salma Hayek Pinault, Olivia Wilde na Hugh Jackman.

Tamasha hilo litaoanekana moja kwa moja kupitia MSNBC na kupitia tovuti za iHeartRadio na Tidal.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents