Burudani

Scorpion Girl wabadili gia angani, sasa wajipanga kuachia albamu mpya ‘Mchepuko Vumbi’

Kundi la muziki la Scorpion Girl ambalo linaundwa na Baby Madaha na Issabela pamoja Kabula baada ya kuhaidi kuachia wimbo ‘Mchepuko Vumbi’, wameamua kujipanga upya na kuja na albamu ambayo imepewa jina ‘Mchepuko Vumbi’.
WhatsApp Image 2016-09-06 at 22.45.36
Scorpion Girl

Akiongea na Bongo5 Jumatano hii, Mmoja kati ya wasanii hao, Issabela amesema tayari wameshaingia studio kwa ajili ya maandalizi ya albamu hiyo.

“Kwa sasa kitu ambacho tunafanya tunajiandaa na uzinduzi wa albamu yetu mpya ‘Mchepuko Vumbi’ tumeshanya nyimbo nyingi, lakini tumeplan kwanza tutaanza tuachia nyimbo mbili kwanza ambazo zipo tayari, ambazo ni ‘Mchepuko Vumbi’ pamoja ‘Mario’ na mwezi wa kumi na moja mwishoni albamu itakuwa tayari,” alisema Bela.

Pia muimbaji huyo amesema tayari wameshaanza kupata show mbalimbali huku wakitarajia kupata show nyingi zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents