Michezo

Serengeti Boys yatoka sare na Korea Kusini watinga nusu fainali mashindano ya (AIF Youth Cup 2016 U-16)

Timu ya soka ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ Mei 19, 2016 wametinga hatua ya nusu fainali baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Korea Kusini katika mfululizo wa michuano maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini India (AIF Youth Cup 2016 U-16).

738X503_51105618573da85489750

Katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa, India, mabao ya Serengeti yalifungwa na Assad Juma katika dakika ya 12 na Maulid Lembe katika dakika ya 87 ambaye alisawazisha baada ya Korea kutangulia kwa mabao 2-1. Matokeo hayo yanaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi tano na kwamba inasubiri matokeo ya mwisho kati ya Korea Kusini na Marekani yatakayotoa mwanga wa timu itakayocheza fainali.

Serengeti Boys watashuka dimbani tena dhidi ya Malaysia Mei 21, 2016,Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 25, 2016 na kabla ya mchezo wa fainali, utachezwa mchezo wa mshindi wa tatu katika uwanja huo huo Tilak Maidan, Vasco, Goa nchini India. India imeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya fainali za kombe la dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents