Habari

Serikali kuwakaba koo madalali feki wa nyumba

Waziri wa ardhi nyumba na makazi, Mh. William Lukuvi,amepiga marufuku vitendo vya madalali kula njama na mabenki kuuza mali za wakopaji wanyonge kinyume na sheria.

4-1-1-1

Alizungumza hayo katika kikao cha madalali kilichofanyika Dar es Salaam, lengo ni kuwaonya madalali wasio waaminifu.

“Baadhi ya madalali hawafuati sheria, wanakwenda kwenye minada kutimiza wajibu, lakini mnununuzi wanakuwa washapewa,” alisema Lukuvi.

“Nyumba yenye thamani ya shilingi 432,000,000 huuzwa kwa shilingi 140,000,000 na bado anatakiwa kulipa gharama zingine. Hali kadhalika shamba lenye gharama ya shilingi bilioni 1 linauzwa kawa shilingi milioni 200 wakati mkopo halisi ulikuwa milioni 400,” alifafanua.

Aidha Lukuvi alisema amepokea kesi zaidi ya 80 za watu walioonewa na madalali hao na zaidi ya asilimia 75 ni wanawake.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents