Habari

Serikali yauomba uongozi wa Agha Khan kujenga hospitali nyingine Dodoma

Serikali imeuomba uongozi wa Agha Khan kujenga hospitali nyingine kubwa mkoani Dodoma ili kuendana na agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli.

pix 4

Akizungumza Jumanne hii jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya jengo la hospitali ya Agha Khan Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alishauri uongozi wa hospitali hiyo kuwa wanatakiwa wajenge hospitali nyingine kubwa mkoani Dodoma ili watoe huduma bora za kiafya na kuboresha huduma hizo.

pix 3

“Kutokana na agizo la Rais wa awamu ya tano la kuhamia Dodoma inabidi na nyinyi mjenge kule kwa kujenga hospitali hiyo serikali itakuwa imeokoa bilioni 20 mpaka 25 kwa ajili ya wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi” ,alisema Mh Ummy Mwalimu.

pix 2

Aliupongeza uongozi wa Agha Khan kwa kuanza kujenga jengo hilo lililogharimu shilingi bilioni 112 ili kuondoa kero kwa wagonjwa wa magonjwa yasiyoambukizwa na kurahisisha huduma na matibabu bora kwa wagonjwa nchini.

pix 1

Naye mwenyekiti wa kamati ya bodi ya hospitali hiyo, Bi Zahra Agha Khan alisema, ” tuna mpango wa kumaliza jengo hilo kwaajili ya kutoa huduma bora za kiafya nchini ili kutokomeza maradhi ya mara kwa mara pia tuna morali kubwa ya kumalizia jengo hili ili tuweze kuboresha huduma ya afya nchini kwa kutoa tiba zenye uhakika na za kisasa.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents