Burudani

Rihanna atangaza jina la wimbo wake mpya

Rihanna ametangaza wimbo wake mpya unaofuata na unaopatikana kwenye albamu yake ANTI.

rihanna-puma-fenty

Msanii huyo amepanga kuachia wimbo ‘Love on the Brain’ hiyo ni kwa mujibu wa ujumbe wa msanii huyo aliouweka kwenye mtandao wake wa Instagram.

“#nextsingle,” aliandika kwenye kipande cha video kinachomuonyesha akiwa jukwaani anaimba wimbo huo.

Wimbo wa ‘Love on the Brain’ ni moja kati ya nyimbo 13 za Rihanna ambao zinapatikana kwenye albamu yake ya ANTI. Nyingine ni pamoja na ‘Work’, ‘Kiss It Better’, ‘Needed Me’, ‘Close to You’, ‘Desperado’ na zingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents