Burudani

Wasanii wa bongo tuna ‘fake’ vitu vingi – Kassim Mganga

Msanii wa muziki, Kassim Mganga amesema wasanii wengi wa bongo wana ‘fake’ kuwa na maisha bora wakati hawapo hivyo.
Kassim Mganga

Muimbaji huyo ambaye ni mtunzi mzuri wa nyimbo za mahaba, amesema wasanii wengi ‘wanafake’ maisha yao ili walingane na mastaa wakubwa duniani.

“Mi ambacho nimejifunza, wenzetu hawa’act, wenzetu wako real, ndio maisha yako vile, ukimuona Chris Brown au ukimuona 50 Cent pamoja na umri wake aliokuwa nao leo, anaonesha magari yake na nini na nini, watu wapo kwenye ushindani wa biashara kubwa sana, kwa hiyo anachokifanya kina mantiki, sisi tumekuwa tuna’fake vitu vingi havipo real, lakini tunataka tuwaoneshe kwenye mitandao, tunadanganya, tunawadanganya sana mashabiki wetu, mashabiki wanatuona si watu ambao tuna maisha makubwa sana, wakati haiko hivyo kiuhalisia,” Kassim Mganga alikiambia kipindi cha Planet bongo cha EA Radio.

Pia muimbaji huyo amewataka wasanii wachanga kuacha kuiga maisha ya mastaa wa bongo ambao wanafake maisha yao ili kuwadanganya mashabiki wao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents