Michezo

Sharapova abainika kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni afeli vipimo Australia Open

Mcheza wa Tenesi Maria Sharapova nyota namba moja wa zamani amethibitisha kushindwa vipimo baada ya kubainika alitumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni katika michuano ya wazi ya Australia Mwaka huu.

Sharapova raia wa Urusi mwenye miaka 28 amepimwa na kubainika kutumia dawa za meldonium, ambazo amekua akitumia toka mwaka 2006.

31F7A62800000578-3481259-image-a-70_1457395838029

Akiwa ni mshindi wa Grand Slam kwa mara tano, alisema hakujua vikwazo atavyokuja kutana navyo. kwa miaka 10 nimekua nikitumia dawa zinazoitwa mildronate nikipewa na daktari wangu na familia yangu.

Katika siku chache zilizopita nimepata barua kutoka ITF (shirikisho la tenesi la kimataifa) na nikagundua kuwa dawa hizo zina jina jingine la meldonium,

“Ni muhimu sana kuelewa kwa miaka 10 dawa hizi hazikua kwenye orodha ya shirika la kudhibiti matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni (Wada). “Lakini sheria zilibadilika mwezi January na kuzifanya dawa za meldonium kukatazwa, kitu ambacho sikufahamu, mwezi Desemba tarehe 22 nilipata barua pepe toka Wada kuhusu mabadiliko kwa dawa zilizokatazwa, ila sikufungua hiyo linki”.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents