Habari

Show ya JB Mpiana, Paris yazuiliwa, sababu za kisiasa zatajwa, atishiwa maisha

Mwanamuziki wa Congo, JB Mpiana na bendi yake ya Wenge Musica BCBG wamejikuta katika wakati mgumu baada ya show yake iliyokuwa ifanyike juzi December 21 jijini Paris, Ufaransa kuzuiliwa.

JB-Mpiana1

Kuzuiliwa kwa show hiyo kulitangazwa Alhamis iliyopita kupitia website ya ukumbi wa La Villette wa jijini Ufaransa ambako show hiyo ilikuwa ifanyike. Hilo lilikuwa pigo kwa Mpiana na bendi yake kwakuwa walikuwa wameshajiandaa kuondoka baada ya kupokea visa 40.

Msemaji wa bendi hiyo, Roger Ngandu ameuambia mtandao Jeune Afrique kuwa wamefedheheshwa na hatua hiyo na kwamba JB Mpiana alikuwa hana taarifa za kusimamishwa kwa show hiyo na sababu zake. Tangu kutangazwa kwa show hiyo jijini Paris, makundi ya wanaharakati ya Kikongo yaliyopo barani Ulaya, yametoa vitisho vya kumuua JB Mpiana akitumbuiza.

Kundi la watu kutoka Brussels na London lilisafiri hadi Paris kukwamisha maandilizi ya show hiyo.

Kwa takriban miaka mitano wanaharakati hao wanaojiita ‘combattants’ wamempiga marufuku JB Mpiana kutumbuiza kwenye majiji ya Ulaya. Wanamshutumu mwanamuziki huyo kwa kutokuwa karibu na masuala ya wananchi wa Congo na kwa ukaribu wake na rais wa DRC Joseph Kabila.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents