Burudani

Sifikirii kutoa tena album, nikitoa itapatikana mtandaoni pekee – Matonya

Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Seif Shaaban maarufu kama Matonya, amesema hakuna tena uwezekano wa kutoa album za muziki na kwamba pesa za msanii kwa sasa zipo kwenye mitandao ya kuuza nyimbo.

Matonya

Matonya ameiambia Bongo5 kuwa yeye ni mmoja wa wasanii waliokata tamaa kutokana na soko la album kufa.

“Uwezokano hakuna tena wa kutoa album kwa sasa,” amesema. “Dunia inavyokwenda kuna vitu vingi vipya vimekuja. Sasa hivi tumeingia kwenye mfumo wa dijitali baada ya kutoka kwenye mfumo wa analojia. Lile soko lilipita halikuwa zuri sana kwa sababu ya uvujifu wa kazi za wasanii Mtu alikuwa anaweza kununua CD moja akaikopi na kuwanufaisha zaidi ya watu 50. Kwahiyo ni hasara kubwa sana kwenye taifa na kwa wasanii,” ameongeza.

“Mimi nimejaribu kuachana na hiyo biashara na sio mimi tu, wasanii wengi tu hawana mpango tena na album kwa maana kazi haitulipi sana. Sasa hivi pesa zetu zipo kwenye mitandao ya kuuza nyimbo. Sasa hivi kwa njia ya mitandao unaweza sambaza kazi zako duniani kote kwa muda mchache, kwahiyo sasa hivi soko limekuwa zuri kwenye mtandao,” amesisitiza.

Pia Matonya amesema kuwa video ya wimbo wake ‘Mule Mule’ inafanya zaidi vizuri nje ya mipaka kuliko nchini.

“Mule Mule simu za nje zimekuwa nyingi sana,” anasema. “Watu wa nje wameielewa kazi zaidi na hapa ndani video naona imefanya vizuri sana. Kwahiyo kwangu mimi naona ni mwanzo mzuri kwa msanii kama mimi ambaye nilihama kutoka analojia nakuja dijitali. Hii ni dalili nzuri ya muziki wangu. Naomba watu wangu waendelee kuuunga mkono muziki wangu ili tufike mbali zaidi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents