Burudani

Stamina awashirikisha rappers watano kwenye remix ya ‘Father Like Son’

Rapper wa Morogoro, Stamina amesema anajipanga kutoa remix ya wimbo ‘Father like Son’ aliyowashirikisha Nikki Mbishi, Chidi Benz, Fid Q, Songa na Noorah.

Stamina

Stamina ameiambia Bongo5 kuwa wimbo ‘Father Like Son’ haujafeli ila amefanya remix ili kuungana na wasanii wengi zaidi kupata kitu kizuri zaidi.

“Lengo letu ni kukuza nyimbo pia nilikuwa natamani kufanya ngoma ya pamoja na wasanii kama Chid Benz na wengine. Kwahiyo kuwapata kwa pamoja na kufanya nao kitu kwa pamoja ndio jambo zuri,” amesema Stamina.

“Nilikuwa sijawahi kufanya kazi na Noorah, Chidi Benz, huu ndo wakati wake na sio wimbo umeshindwa kufanya vizuri. Kuna nyimbo ngapi zinahit uchochoroni hazifanyi vizuri redioni? Wasanii wangapi wanaanza kuhit mtaani ndo wanaingia redio? Kwahiyo hiyo inaonyesha kabisa muziki mzuri sio lazima upigwe redioni. Kitendo cha mtu kuwa na nyimbo yako na akasikiliza ni kukubalika tosha,” ameongeza.

“Ulaya wana nyimbo za mtaani, nyimbo za redioni na zote zina nafasi katika muziki. Na sio sio kila kinachopigwa redioni ni kizuri. Unajua Tanzania ni kubwa sana na tuna redio nyingi. Huenda redio ya karibu yako ndo haipigi lakini redio nyingine zinapiga. Kwahiyo mashabiki wangu wasubirie remix ya wimbo na utatoka pamoja na album yangu mpya ‘Mount Mount Uluguru’ siku ya Jumatano.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents