Burudani

Siku ya kuachiwa filamu ya maisha ya Tupac yatajwa rasmi

Baada ya kuisubiri kwa muda mrefu hatimaye siku rasmi itakayotoka filamu yas maisha ya Tupac Shakur ‘All Eyez On Me’ imetajwa.

tupac-shakur-camo

Filamu hiyo imepangwa kuachiwa siku aliyozaliwa rapper huyo Juni 16, 2017. Kwenye filamu hiyo Demetrius Shipp ameigiza kama Tupac huku Danai Gurira akiigiza nafasi ya Afeni Shakur ambaye ni mama mzazi wa rapper huyo ambaye alifariki mwezi Mei, mwaka huu kwa tatizo la mshtuko wa moyo.

Wakati huo huo Jamal Woolard ameigiza kama The Notorious B.I.G, Dominic L. Santana ameigiza kama Suge Knight.

Tupac alifariki dunia Septemba 13, 1996 kwa kupigwa risasi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents