Habari

Sikuwahi kuolewa, najua tunakokwenda wanawake watakuwa na nguvu kuliko akina baba – Mh. Anne Makinda (+video)

Aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Anne Makinda ameelezea historia yake fupi ya maisha toka enzi anasoma hadi kuja kufanikiwa kuwa kiongozi mkubwa bungeni.

Image result for anne makinda
Mhe. Anne Makinda

Mhe. Makinda amesema maisha yake yote yalikuwa bungeni na kipindi hicho amesema kuwa alikuwa na fujo sana kuliko hizi ambazo zinafanywa na baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani bungeni.

Mimi maisha yangu yote yalikuwa bungeni, mimi mwenyewe kama kuwa mtu wa fujo i was of those.. nilikuwaga backbencher nilikuwa na fujo nawambia ndugu zangu akina Tundu Lissu kuwa kwanza nyie hamuwezi kunifikia mimi,“amesema Anna Makinda.

Akielezea upande wa mahusiano Bi. Makinda amesema yeye hakuwahi kubahatika kuolewa na amewaasa wanawake waliokwenye ndoa kuwa makini sana pale wanapopata mafanikio kwani ndio kipindi cha kushirikiana karibu sana na wanaume zao ili kufika mbali.

Mimi sikuwahi kuolewa lakini nilipopata mtoto wangu, aliyenisaidia sana ni dada yangu. Kwa hiyo nikiwa shuleni tu IDM nikipata ile shilingi 20 kumi napeleka kwa dada, 10 nabaki nazo kwa hiyo toka huko nilikuwa nafanya kazi I have to survive .“amesema Bi. Makinda  na kusisitiza jambo kwa wanawake walioolewa.

Tunakokwenda najua kabisa akina mama watakuwa na nguvu zaidi kuliko akina baba, na ndio maana nawa-advice pia tujifunze kuwapenda hawa watu. Kwa sababu kama wewe ni Couple umeolewa halafu unakuwa successful kuliko mume wako, usipoweza kumeneji hiyo anaweza kukuharibia hata wewe, ni vizuri kumshirikisha ikawa ile successful yako ikawa ni part ya familia yako au  successful ya couple yenu,“amesema Anne Makinda akielezea historia yake kwenye mahojiano na TGNP Mtandao, tazama video hapa chini.

Mhe. Anne Makinda ndiye mwanamke wa kwanza nchini Tanzania kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na alishawahi kuhudumu pia kwenye shirika la UNICEF .

Related Articles

60 Comments

  1. Mbona lishatimia hilo.si unaona siku hizi Wanaume ndo wanaongoza kwa kuhama vyama eti hawapati malezi mazuri.!!😀😀😀 Ila huyo Mh.Makinda hata kama angeolewa labda aolewe na Mjeshi maana sio kwa sura hiyo!!

  2. Mwanamke kujikomaza komaza kama mgambo wa jiji akuoe nani!??
    Mwanamke unapaswa ujiregeze kidogo watu wavutike……!!!
    Ata uwe na sura mbovu vp ukivaa stara na kujiregeza watu watakuja tu kutangaza posa….
    Pesa hazimpi heshima mwanamke ila ndoa humfanya mwanamke kuwa bora….!!!

  3. Kama hajawahi kuolewa atakuwa kubwa la wadhinifu alafu afute iyo kauri yake kama ipo siku wanawake watakuwa na nguvu kuliko sisi wanaume ivi unatujua vizuri wewe wanaume tunatisha Kila siku tuna tumia fomesheni mpyaaaa

  4. hiyo nguvu ya kupandikizwa hauoni waya umeshakatwa tafuta kijana wa kukupoza machungu we fala mjanja hadi dunia inakwisha hamtapata uwezo na nguvu kama mwanamume umekimbia kuolewa unadanganya wenzako eti tutakuwa na nguvu nyoooooooooooooo… Njoo uone wasimbe wenzako wanavyoshindia andazi moja na maji uspotoshe umma…

  5. Daaah ww kukaa kote crkalin nafas zote uzopewa alafu eti hujawah olewa io ni aibu kubwa kwako na unazalilisha wenzako hujui tuu. Labda ungesema huna hisia za kimapenzi au km ulitumia mirungi hapo sawa. Km uliota mwanamke atakuwa na nguvu kumshinda mwanaume sahau kuna gape kubwa ata ww unalijua. Hv hujiuliz kwann kwny maandiko hakuna nabii mwanamke na hata vitan ni nadra sana kuona front line kuna askar mwanamke? Mungu akusamehe labda umejisahau

  6. Moja wapo ya stress za kutokuolewa ndio hiii.ewe binti wa sasa muombe Mungu akupe wako usije ukawa na stress kama za huyu bibi na kuropoka non sense.kumbe si watu wazima wote wenye hekima

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents