Bongo Movie

Timoth Conrad amcharua Gabo, Duma na Aunt Ezekiel kwa madai wametoa filamu mbovu!

Weekend hii muigizaji Duma alifanya uzinduzi wa filamu yake mpya ‘Nipe Changu’na kuhudhuriwa na mashabiki wengi ambapo kiingilio kilikuwa ni tsh 50000 kwa VIP na kwa watu wa kawaida tsh 30000.

Uzinduzi huo ni wiki chache toka Gabo Zigamba na yeye azindue filamu yake ya Sumu na kuhudhuriwa na mashabiki wengi.

Mtayarishaji wa filamu, Timoth Conrad ambaye anafanya kazi chini ya kampuni ya Timamu, amesema baada ya kuangalia filamu hizo pamoja na filamu ya muigizaji Aunt Ezekiel itwayo Mama, amedai filamu hizo zina ubora mbovu na haziwezi kuliinua soko la filamu Tanzania.

Timo baada ya kuangalia filamu hizo, alindika “Naiona DALILI MBAYA kwa wapenzi na watazamaji wa bongo movies ambao kila wakati wanajitokeza kwenye uzinduzi kila unapotangazwa! Lakini Mara nyingi watazamaji wanakosa kuridhishwa na ubora wa filamu iliyowafanya wakaacha shughuli zako, wakatumia gharama zao kuhakikisha wanafika kutoa support kwa kazi za nyumbani!.

Tukubali, tukatae asilimia kubwa ya walioziona filamu za MAMA (Anti Ezekiel) SUMU (Gabo Zigamba) pamoja na NIPE CHANGU (Duma) iliyozinduliwa Jana hawajaridhishwa na ubora wa filamu hizo!.

HATARI kwa sasa imani kwa watazamaji bado IPO lakini wakati mfupi ujao imani itapotea na hapo sasa hata ikitangazwa itazinduliwa filamu la kimataifa sijui la kidunia hakuna atakayekuja hata kwa BURE!.

MUHIMU washkaji zangu, bongo movies wenzangu, tusichukulie poa. Muda wa watazamaji ni MALI tusipende kuonewa huruma na kwa kulalamika eti “ooh wapende kazi zetu, wasupport vya nyumbani” NOOOO! Watazamaji wanataka kitu kizuri nao wajivunie kua tasnia ya BONGO MOVIES inakua. Washkaji zangu msidhani pale kwenye uzinduzi wanakuja watu wa kawaida tuu kuna wengine ni WAWEKEZAJI mabosi wameshawishika na wanataka kuwekeza na wanakuja kutazama ili kutoa support kwenye movie industry matokeo yake wanakuta MOVIE MBOVU, Haieleweki Director haelewi alichokifanya, Actor kapuyanga, story manyanga matupu, Dah!.

Najua kuna wengine watasema oooh “unaongelea movie za wenzako na wewe zindua yako tuone” ila jibu langu kwao nikua hapa tunapojadili faida ya BONGO MOVIES nzima sio muda wakutambiana nani movie yake kali na nani movie yake mbaya!
#MudaWaKusemaUkweli
#UkichukiaZimaData,”

Related Articles

3 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents