Michezo

Simba Day Septemba 19, wenyewe wathibitisha

Klabu ya soka ya Simba imetangaza rasmi tarehe itakayofanya tamasha lao kubwa lijulikanalo kama Simba Day ambalo hutumika kutangaza wachezaji wapya.

Kwa mujibu wa Miamba hiyo ya soka Afrika siku ya Jumapili Septemba 19, 2021 ndiyo tamasha hilo litafanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mara kadhaa tamasha hilo la utambulisho wa wachezaji wapya waliyosajiliwa kwaajili ya msimu mpya, hunogeshwa na burudani mbalimbali ya muziki.

Kulikuwa na tetesi kadhaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na kutofanyika kwa tamasha hilo msimu huu huku wengine wakihusisha na aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo Haji Manara kuhamia Yanga.

Lakini hata hivyo Mabingwa hao wa Nchi Simba SC wamethibitisha rasmi kuwepo kwa tamasha hilo msimu huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents