Michezo

Simba SC kuifuata Njombe Mji wikiendi hii

Kikosi cha klabu ya Simba kinatarajia kusafiri siku ya Jumamosi kuifuata timu ya Njombe Mji kwenye mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania Bara utakao pigwa Aprili 3.

Simba SC itaondoka jijini Dar es Salaam Jumamosi hii kupitia Iringa ambapo itaweka kambi ya siku mbili kisha Jumatatu kuanza safari.

Baada ya mechi hiyo kikosi hicho chenye maskani yake mitaa ya  Karia Koona kitajiandaa na mchezo wake ujao dhidi ya Mtibwa Sugar Aprili 9 kisha kuikabili timu ya Lipuli FC Aprili 20 kabla kuivaa Yanga SC Aprili 29.

John Bocco, Salim Mbonde pamoja na Haruna Niyonzima ni sehemu ya wachezaji wanao fanya mazoezi na kikosi cha Simba SC katika uwanja wa Boko jijiini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents