Michezo

Simba waibuka mshindi wa Nani Mtani Jembe 2014

Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba imemalizika kwa timu ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa bila katika mechi iliyochezwa ndani ya uwanja wa Taifa.

Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kwa makini

Simba ilipata bao la kwanza kupitia Awadh Juma ndani dakika ya 30 na baada ya hapo Elias Maguri ndani ya dakika ya 41 aliiipatia Simba goli la pili mpaka mpira unamalizika na kuwafanya Simba kuibuka na ushindi huo.

Simba iliyoibuka na ushindi huo imekabidhiwa kombe la Nani Mtani Jembe pamoja na kitita cha jumla ya shilingi milioni 92,590000, ambapo milioni 77,590,000 zilipatikana kwa mashabiki wa Simba kupiga kura na milioni 15,000,000 ni za ushindi wa uwanjani.

Yanga ambao ni washindi wa pili wameibuka na kitita cha milioni 7,400,000, milioni 5 za mshindi wa pili baada ya kufungwa na Simba na milioni mbili laki nne ni kutokana na kura zilizopigwa na mashabiki wa Yanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents