Burudani

Sina ushikaji na Mkaliwenu Nyimbo yake Siijui angetoa movie sawa ila sio muziki – Bwana Mjeshi (VIDEO)

Sina ushikaji na Mkaliwenu Nyimbo yake Siijui angetoa movie sawa ila sio muziki - Bwana Mjeshi (VIDEO)

Mchekeshaji kutoka katika kundi la Timamu Bwana Mjeshi amefunguka yote baada ya kupiga stori na Bongo Five juu ya Ukaribu wake na Mchekeshaji mwenzake Mkaliwenu.

Bwana Mjeshi amefunguka hayo baada ya kuongea kuhusu mipango yao ya kazi wao kama Timamu na kusema kuwa wana mipango mikubwa sana katika uchekeshaji pia katika Muvi kwani wanaweza kufanya vitu vikubwa sana hata kupita Muvi ya Black Panther.

Lakini pia aliongelea ukaribu wake na rafiki yake wa muda Mkaliwenu na kusema yeye akikutana na Mkaliwenu wanaongea ila sio ushikaji wa kihivyo

Bwana Mjeshi aliongeza “Mimi na Mkaliwenu Ushikaji ulishakufaga ingawa nikikutana nae naongea nae ila sio ushikaji wa kupigiana na simu au ushikaji wa kikazi hapana”

Mkaliwenu alifanya kazi pamoja na kundi hilo la Timamu kwa kipindi cha nyuma kwa mafanikio makubwa lakini sasa kundi hilo limebakiza washiriki wakuu watatu ambao ni Bwana Mjeshi,Ebitoke pamoja na Masai au Mr Beneficial.

 

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents