Michezo

Singida United yatinga ligi kuu na neema

Klabu ya soka ya Singida United ambayo, imepanda ligi kuu soka Tanzania bara na hivyo kutarajia kushiriki kwa mara ya kwanza katika msimu mpya wa ligi, imepata msaada kutoka Benki ya NMB, ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10 .

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Richard Makungwa alisema msaada huo umelenga kuisaidia timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa kwa ligi.

“Tumetoa msaada huu kwa timu ya Singida United kwa ajili ya maandalizi ya ligi hiyo na hii ni kawaida yetu kusaidia timu mbalimbali pale tunapopata nafasi” alisema Makungwa.

Makungwa alisema, licha ya benki hiyo kufanya shughuli za kibenki pia imejikita kuinua michezo nchini kwa kutoa msaada wa vifaa vya michezo.

Alitaja vifaa walivyotoa kama msaada kwa timu hiyo ikiwa ni pamoja na viatu vya mpira wa miguu, jezi na mipira vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 10.

Katibu wa timu hiyo Abdurahman Sima alisema vifaa hivyo walivyopata vitatumika kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo.

“Tunaishukuru benki ya NMB kwa msaada huu tunaomba wadau wengine kuiga mfano wa benki hii ” alisema Sima.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents