Burudani

Single Mtambalike – Kabla ya kuijibu barua ya uteuzi ya waziri nilizingatia mambo haya (+Video)

Single Mtambalike - Kabla ya kuijibu barua ya uteuzi ya waziri nilizingatia mambo haya

Msanii wa Bongo movie na mjumbe wa kamati ya Baraza la sanaa taifa (Basata) aliyeteuliwa na Waziri wa habari Utamaduni sanaa na michezo Dkt.Harrison Mwakyembe, Single Mtambalike kwa jina maarufu la kisanaa Richie amefunguka na kuweka wazi dhamira yake baada ya kuteuliwa na Mhe.Waziri.

Richie amefunguka juu ya uteuzi wake wakati anapiga stori na Bongo five na kusema kuwa “Na sisimamii sanaa ya filamu tu,nikiwa pale ntasimamia sanaa zote Uchoraji,Uchongaji,Uigizaji,Uimbaji chochote kinachohusu sanaa ndio ntasiamia nikiwa pale kwahiyo sio kazi ndogo”

Pia ameongeza “Kabla ya kujibu barua yangu niliyoteuliwa niliangalia kwanza kama nitaweza kumudu vitu vyote na pia kuangalia muda wako sio kuchukua tu madaraka ingali hutakuwa na muda wa kuyafanyia kazi”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents