Habari

Siri ya viongozi wa ACT Wazalendo kukimwaga chama hicho yafichuka (+video)

Baada ya kutangaza kuachia ngazi ya uongozi wa Chama cha ACT Wazalendo kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa wa chama hicho, Ndg Samson Mwigamba leo Alhamisi ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Samson Mwigamba

Ndg Mwigamba amesema kuwa yeye na wenzake akina Prof. Kitila Mkumbo na wengine  wameamua kuachana na ACT Wazalendo baada ya kuona baadhi ya viongozi wakichepuka na kufanya mambo yaliyo nje ya misingi ya chama huku chama kikibaki kama jahazi lililochanika tanga na kukosa mwelekeo.

Kwa kuzingatia hali ilipofikia ndani ya Chama cha ACT Wazalendo, baadhi yetu tumeamua kujivua uongozi na uanachama kabisa. Uamuzi huu tumeufikia baada ya kuamini  na kushuhudia kuwa uongozi wa chama hiki unachepuka kwa kasi mno nje ya misingi ya chama, na sasa chama kimebaki kuwa jahazi lililochanika tanga na kukosa muelekeo na hivyo kubaki kuyumbishwa kila upande kutegemeana na mawimbi ya bahari.“amesema Mwigamba leo kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari.

Hata hivyo, kiongozi huyo wa zamani wa ACT Wazalendo ametoa sababu zingine zilizomfanya ahamie CCM, kuwa  ni uwiano wa sera na falsafa za Chama cha Mapinduzi na ACT Wazalendo, pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kupambana na rushwa.Tazama video yake hapa chini akifunguka zaidi maamuzi yake ya kuhamia CCM

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents