Burudani

Siwezi kuimba wimbo utakaomkosea heshima mama yangu – Alikiba

Staa wa muziki Ali Kiba amesema mama yake ni mmoja kati ya mashabiki wa muziki wake hivyo kamwe hawezi imba nyimbo ambazo zina matusi ndani yake.

Muimbaji huyo ambaye aliachia video ya wimbo ‘Lupela’ hivi karibuni, ameiambia Bongo5 kuwa tayari ana mashabiki wake ambao wanajua anaimba muziki wa aina gani hivyo hawezi kuwadisappoint.

“Toka nimeanza kufanya muziki mama yangu anausikiliza, yaani hata kama nimetoka kurekodi studio nikawa naisikiliza nyumbani, utasikia baadae anaimba,” alisema Ali Kiba.

“Kwahiyo wakati natafuta njia ya kutoka mama yangu nyimbo zangu zote alikuwa anazijua. Lakini aniambii, najua anafurahia muziki wangu, ni kitu ambacho kinanifanya niimbe nyimbo ambazo kila mmoja anaweza sikiliza, kwa sababu siwezi kuimba nyimbo ambazo zitaweza kumkosea heshima mama yangu kwa sababu ni fan namba moja, hamna matusi wala nini,” aliongeza Ali Kiba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents