Michezo

Stars kutupa karata yake ya kwanza CHAN leo

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo inatarajia kuingia uwanjani kuanza safari ya kusaka tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).

Timu ya taifa ya Tanzania(Taifa Stars) ikiwa katika mashindano ya Cosafa Castle Cup  Julai 02 mwaka 2017  na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu kwa kuifunga Lesotho

Stars itajitupa uwanjani kuvaana na timu ya taifa ya Rwanda (Amavubi) bila kujali rekodi ya matokeo mazuri waliyopata katika michuano ya COSAFA iliyomalizika hivi karibuni huko nchini Afrika Kusini.

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga, amesema kikosi chake amekiandaa vyema kuhakikisha leo wanapata matokeo mazuri.

Kocha huyo aliendelea kwa kusema kuwa kikubwa katika mazoezi alikuwa anawajenga wachezaji kiakili na kujipanga kutowadharau wapinzani wao ambao nao wanataka kupata matokeo.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents