Habari

Swahili Fashion Week & Awards wamekuja na tuzo za muziki (Video)

Jukwaa kubwa la maonyesho ya mavazi Afrika Mashariki na Kati la “Swahili Fashion Week & awards”(#SFW2020) limepanga kufanya maonyesho yake tarehe 4,5 & 6 Desemba mwaka huu, Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam na linatarajia kuleta pamoja wabunifu wapatao 45 kutoka nchi za Afrika Mashariki na kwingineko ulimwenguni. Ikiwa imejijengea mafanikio makubwa kwenye maonyesho yake miaka iliyopita, jukwaa la “Swahili Fashion Week & awards” bado linaongoza kwa umahiri katika tasnia hii ya ubunifu wa mavazi.

 

Muasisi wa “Swahili Fashion Week & awards” Mustafa Hassanali ana matumaini ya kuimarisha msingi wa ubora wa jukwaa hilo na kwa shauku kubwa anasema, “Mwaka 2020 umekuwa na changamoto nyingi sana kiuchumi, pamoja na chanagamoto zinginezo zikiwemo janga la homa ya Korona (Covid 19) wabunifu zaidi ya arobaini na tano (45) wanatarajiwa kuonyesha ubunifu wao kwenye jukwaa la mwaka huu. Hii ni kwa sababu ya hatua zenye tija na chanya zilichichukuliwa na kiongozi wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli katika kuthibiti janga hilo.”

Mustafa anaongeza, “lengo la kuendeleza tasnia ya ubunifu Afrika bado linabaki mstari wa mbele, kwa kupitia jukwaa hili na mtandao wake mkubwa wa vyombo vya habari, watumiaji wa bidhaa za ubunifu wa Tanzania, Afrika na ulimwengu kwa ujumla sasa wataweza kuona mbadala wa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje, na kwa wakati wote tumekua tukitilia mkazo thamani ya bidhaa za ubunifu za Afrika kwa kuhamasisha adhana ya “made in Africa” nakutengeneza bidhaa zenye hadhi ya kimataifa kwa misingi ya Kiafrika.”

Maonyesho haya ya wa kumi na tatu(13) ya “Swahili Fashion Week & awards” yataendelea kuwa kioo kwa maonyesho mengine ya mavazi Afrika kwa wabunifu wa Kitanzania, ukanda wa Afrika Mashariki hata wale wa kimataifa kwa mvuto na mandhari yake ya kipekee inayoendana na kauli mbiu ya jukwaa ya Tambua Kinachoipendezesha Afrika “Discover What Makes Africa Beautiful.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents