Habari

Taasisi za fedha zakopesha Bilioni 59.2 kwa wananchi

Serikali imesema kuwa Bilioni 59.2 zimekopeshwa na Taasisi za Fedha kwa wananchi kupitia hati za kimila katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Akijibu swali la Venance Mwamoto mbunge wa Kilolo (CCM) leo Bungeni, Jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anjelina Mabula amesema kuwa wananchi wameweza kutumia hati za kimila kujipatia mikopo kutoka Benki mbalimbali ikiwemo NMB PLC, CRDB PLC, Stanbic Bank, SIDO na PSPF.

“Natoa rai kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika miradi ya utoaji wa Hati za Kimila inayotekelezwa katika maeneo yao ili ziweze kuwanufaisha kwa ustawi wa kiuchumi na kijamii,” alisisitiza Mhe. Mabula

Mabula amesema kufikia mwezi Machi, 2018 jumla ya hatimiliki za kimila 56,506 zimeandaliwa katika maeneo mbalimbali nchini ambapo wananchi katika maeneo hayo wamenufaika kiuchumi kutokana na mikopo waliyopata kutoka taasisi za kifedha.

Aliongeza kuwa kuna faida nyingi za Hati ya Kimila ikiwemo usalama wa milki, kupunguza migogoro baina ya watumiaji wa ardhi, kutumika kama dhamana katika taasisi za fedha na vyombo vya kisheria.

Aidha Mhe. Mabula alitoa rai kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika miradi ya utoaji wa hati za hakimiliki za kimila inayotekelezwa katika maeneo yao ili ziweze kuwanufaisha kwa ustawi wa kiuchumi na kijamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents