Habari

Taiwan yapeleka msaada India

Shehena ya kwanza ya msaada wa Taiwan kwa India kusaidia nchi hiyo kukabilina na wimbi la maambukizi ya virusi vya corona imeondoka leo kwenda mjini New Delhi ikiwa na mashine 150 za kupumua na mitungi 500 ya hewa ya Oksijeni.

Taiwan stands with India: President Tsai Ing-wen offers to provide help amid COVID crisis

Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen

Wizara ya mambo ya kigeni ya Taiwan imesema shehena hiyo iliyobebwa na shirika la ndege la China imeondoka mjini Taipei leo asubuhi na itapokewa na shirika la msalaba mwekundu nchini India.

Wakati India kama yaliyo mataifa mengi duniani haina uhusiano rasmi wa kidiplomasia na Taiwan ambayo China inadai kuwa ni sehemu ya himaya yake, pande hizo mbili zimejenga urafiki katika miaka ya hivi karibuni kutokana na ajenda ya pamoja ya kuipinga Beijing.

Mataifa kadhaa duniani yanachukua hatua ya kuisaidia India kukabiliana na janga la Covid-19 baada ya kurekodi idadi kubwa ya maambukizi katika siku za karibuni ikiwemo visa vipya 400,000 jana Jumamosi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents