Habari

Tanzania kutengeneza dawa za ARV

Kiwanda cha kutengeneza dawa za binadamu cha ZENUFA, kipo kwenye majaribio ya kutengeneza dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa Ukimwi (ARV) ili kuwasaidia waliopata maambukizo ya ugonjwa huo.

Na Hellen Mwango

 

 

 
Kiwanda cha kutengeneza dawa za binadamu cha ZENUFA, kipo kwenye majaribio ya kutengeneza dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa Ukimwi (ARV) ili kuwasaidia waliopata maambukizo ya ugonjwa huo.

 

Kiwanda hicho kinategemea kupata kibali cha kuanza kutengeneza na kusambaza dawa hizo kati ya Agosti na Septemba mwaka huu, kutoka katika Shirika la Kimataifa la Afya (WHO), nchini Geneva.

 

Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Kamal Kotecha, alikuwa akimueleza balozi wa Marekani nchini, Bw. Mark Green, alipotembelea kiwanda hicho.

 

Bw. Kotecha alisema, mbali na ARV pia wanatengeneza dawa za kutibu maradhi ya malaria, kisukari na magonjwa mengine.

 

Alisema kwa sasa wako katika majaribio ya kutengeneza dawa za aina nne, chini ya uangalizi wa daktari kwa lengo kuangalia uhimili wake ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFA) itatoa kibali kwa ajili ya kuanza kuingizwa sokoni kwa matumizi ya binadamu.

 

Bw. Kotecha alizitaja dawa hizo kuwa ni, Lamivudine, Stavudine, Zidovudine na Lamivudine-Stavudine.

 

Aliongeza kuwa pamoja na majaribio, uzalishaji huo utaongeza kipato kwa njia ya kuwapa ajira wazawa ili wajikwamue katika maisha yao ya kila siku.

 

Naye, Bw. Green, alisema amefurahi kuona Tanzania iko mstari wa mbele katika kupambana na kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo hivyo ni wazi nchi inaingia katika ushindani kwa njia ya kutengeneza dawa za kuwasaidia wenye maradhi hayo.

 

Alisema kuwa kuingia katika ushindani ni kupiga hatua moja kwenda nyingine hivyo kuna urahisi wa kuingia kwenye ushindani na kupenya katika soko la nchi za Ulaya na kwamba itaiongezea nchi kipato.

 

 

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents