Michezo

Tanzania yaporomoka viwango vya FIFA

Timu ya taifa Tanzania imeporomoka katika viwango vya ubora wa soka duniani ‘FIFA Ranking’ vilivyotolewa  mapema hii leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu DUlimwenguni ‘FIFA’.

Tanzania imeporomoka kwa katika viwango hivyo kwa kushika nafasi ya 125 ikitoka 120 iliyokuwa hapo awali.

Timu za soka za mataifa ya Kenya na Tanzania zimeshuka kwenye orodha ya kila mwezi ya viwango vya soka duniani inayotolewa na Fifa.

Wakati majirani zao Kenya ikishuka kwa nafasi sita hadi nambari 88 duniani timu ya taifa ya Rwanda wamepanda nafasi moja hadi nambari 118, huku DR Congo wakishuka nafasi 14 hadi nambari 42.

Kwa timu za taifa za Afrika Mashariki nchi ya Uganda imeendelea kuwa tishio katika viwango hivyo vya FIFA baada ya kupanda kwa nafasi mbili nakushika nafasi ya 71.

Timu ya taifa ya Burundi wakikwea kwa nafasi mbili na kushika nafasi ya 129 wakati wababe wa soka la Afrika timu ya Misri wakiongoza kwa kuwa nafasi ya 30 ilhali ikiwa imeporomoka kwa nafasi 5.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents