Burudani

Tarajia kolabo hizi kubwa za kimataifa mwaka huu kutoka kwa Wakazi

Mwaka 2017 rapa, Wakazi aliahidi mashabiki wake kuwa mwaka huu ataachia album yake ya KISIMANI ambayo itakuwa na ngoma 18 alizowashirikisha baadhi ya wasanii kama One The Incredible, Barakah The Prince, Ayler na wengine kibao.

Sasa Wakazi amesema mwaka huu baada ya kuachia album hiyo ndio utakuwa mwanzo wa kufungua kolabo na wasanii wa kimataifa kutoka nje ya Tanzania.

Wakazi amesema kwa sasa anashughulikia album yake ili aweze kuikamilisha na kuiachia kwa mashabiki wake lakini tayari kuna wasanii  wakubwa ameshafanya nao kazi bado muda tu kukamilisha baadhi ya vitu.

Akitaja wasanii hao, Wakazi amesema ni M.I Abaga na Ice Prince wote kutoka Nigeria  na kudai kuwa ameshafanya nao kazi wakaishia njiani ila mwaka huu wanamalizia.

Baada ya album ya Kisimani kutoka mwaka huu nitarudi kwenye kolabo za kimataifa, kwani tayari nimeshafanya kazi na M.I na Ice Prince zikaishia njiani naamini huu mwaka tutazimaliza,“amesema Wakazi kwenye mahojiano yake na Bongo5.

Wakazi ni moja ya Marapa wa Tanzania ambao album yake inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa hip hop nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents