Burudani

Target ya muziki wa Darassa sio kufanya show nyingi za kawaida – Hanscana

Mwongozaji wa video za muziki nchini ambaye pia ni mmoja kati ya mameneja wa rapper Darassa, Hanscana amefunguka na kuzungumzia kwanini rapper huyo hajafanya show nyingi kama watu walivyotarajia baada ya wimbo wa rapper huyo ‘Muziki’ kufanya vizuri zaidi katika vituo mbalimbali vya redio na runinga.

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Hanscana amedai lengo lao kwa sasa sio show hizi za kawaida ambazo zinajitokeza kwani wanampango wa kufanya matamasha makubwa ambayo yanaweza hata kufanyika katika viwanja vikubwa.

“Kata kabla ya Darassa kuachia wimbo Muziki alikuwa sio msanii wa show show hizo za kaiwada, sisi tuna maengo ya kufanya muziki mkubwa, Muziki ni moja kati ya project ambazo ziliandaliwa ili kumfikisha Darassa sehemu fulani bado ndani tuna kazi nyingi sana, tumeshazalisha content ya kutosha,” alisema Hanscana. “Show zinakuja lakini sio wakati wake tunashindwa kuzikataa watu wasije wakaona tunazingua au tujidai pia huwezi kukaa muda mrefu bila show hata mashabiki wataona kama unazingua,” alisema Hanscana.

Aliongeza, “Malengo yetu kwa sasa ni kutengeneza content ambayo itatuwezesha kufanya matamasha makubwa na tayari tumefikia katika hatua nzuri kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula kwa ajili ya muziki nzuri,”

Meneja huyo amedai Darassa hakufanya show nyingi hata baada ya wimbo ‘Muziki’ kufanya vizuri kwa kuwa target yake haikuwa hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents