Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa hii, Man City yaifanyia umafia United kwa kunasa saini ya Cancelo, Neymar aigomea Real aitaka Barcelona, Draxler, De Ligt, Gueye sokoni

Ripoti zinaeleza kuwa Manchester City imekamilisha dili la kumsajili beki wa kulia wa Juventus, Joao Cancelo. Kwa sasa mabingwa hao wa Premier wapo katika hatua za mwisho za mazungumzo na tayari klabu ya Juventus imekubali dau la pauni milioni 44.

Joao Cancelo was wanted by Manchester United and Manchester City this summer

Cancelo alikuwa akiwindwa na Manchester United na amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kutua Old Trafford lakini ripoti zinasema kuwa tayari ameshakubali kuanguka saini Manchester City.

Mshambuliaji wa Brazil, Neymar amekataa kuelekea Real Madrid na kuiambia Paris Saint-Germain kuwa anataka kuelekea Barcelona tu . (Express)

Tottenham imepewa ofa ya mchezaji wa kijerumani na mshambuliaji wa Paris St-Germain,Julian Draxler,25, kama mbadala wa Christian Eriksen ikiwa mchezaji huyo, 27, ataondoka. (Star)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi Matthijs de Ligt, 19 huenda akachagua kuichezea Paris St-Germain au Barcelona. (Marca)

Mashetani wekundu wanalenga sahihi mbili kubwa mwezi huu.(Sun)

Neymar

Wakati huohuo, kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans,22, ambaye alitumia msimu uliopita akiichezea Leicester kwa mkopo akitokea Monaco, anahitajika Old Trafford ikiwa Paul Pogba, ataamua kuondoka United.(Independent)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Foxes na Uingereza, Harry Maguire, 26,anajiandaa kuikacha Manchester United, na kuwa na mpango wa kwenda Manchester City. (Mail)

Na kiungo wa kati wa Leicester City, James Maddison anataka kuendelea kubaki King Power, ingawa Manchester United na Tottenham zina nia ya kumchukua. (Mail)

Paris Saint-Germain huenda wakatoa ofa kumnasa kiungo wa kati wa Everton, Idrissa Gueye. (Le 10 Sport)

Idrissa Gueye

Everton wameiambia Tottenham wanamtaka beki wa kushoto Danny Rose, 28, ili kumuachia Lucas Digne, 25,aondoke Goodison Park. (Star)

Winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco, 25, karibu atahamia Arsenal kutoka timu ya Dalian Yifang ya uchina.(Mirror)

Mchezaji wa nafasi ya Joachim Andersen,23, huenda akachagua kwenda AC Milan badala ya Arsenal kama meneja wake wa timu anayoichezea sasa Sampdoria, Marco Giampaolo ataamua kuelekea Rossoneri. (Metro)

Schalke wako kwenye kinyang’anyiro cha kupata saini ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi ya Everton Jonjoe Kenny,22, kwa mkopo.(Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Venezuela Salomon Rondon, 29, anajiandaa kuzungumza na Fenerbahce baada ya mipango ya Newcastle kumpata kwa mkopo kutoka West Brom kugonga mwamba. (Sun)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents