Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili hii, Pochettino kutimka Spurs, Mourinho kutua Madrid, Klopp avutiwa na Ujerumani 

Kocha wa timu ya taifa Uingereza, Gareth Southgate anapewa nafasi kubwa ya kuwa mrithi wa Mauricio Pochettino ndani ya klabu ya Tottenham. (Star Sunday)

Wachezaji wa Spurs wameanza kuamini kuwa meneja Pochettino hivi karibuni ataondoka katika klabu hiyo, huku Manchester United ikiwa ndio klabu anayovutiwa nayo. (Sun on Sunday)

Aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho anajitayarsha kurudi Real Madrid, huku rais Florentino Perez akimpanga raia huyo wa Ureno kuichukua nafasi ya Zinedine Zidane. (Sunday Times)

Liverpool inataka kumsajili mchezaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 22 David Neres kutoka Ajax. (Calciomercato)

Liverpool inahofia huenda kocha wake Jurgen Klopp akavutiwa na kuifundisha timu ya Ujerumani baada ya kumalizika kwa kipindi cha mkataba wa meneja Low. (Sunday Mirror)

West Ham ipo tayari kuweka thamani ya £100m kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya England Declan Rice ili kuilemaza Manchester United katika jitihada zake za kutaka kumsajili mchezaji huyo wa miaka. (Sunday Express)Jose MourinhoJose Mourinho anajitayarisha kurudi Real Madrid

Barcelona ipo tayari kufufua azimio lake la kumfukuzia winga wa Chelsea Willian mwenye umri wa miaka 31. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa timu ya Brazil unakamilika mwishoni mwa msimu. (Mundo Deportivo)

Meneja Pep Guardiola anasema Manchester City haitonunua wachezaji wowote mwezi Januari kwasababu klabu hiyo haina pesa. (Sky Sports)

Manchester City inataka kumsajili beki wa kati wa Leicester City mwenye umri wa miaka 23-Caglar Soyuncu. (Fotospor kupitia Metro)

Manchester City imempatia ocha wa Uholanzi Giovanni van ¬Bronckhorst jukumu la ndani ya klabu wakati ikijitayarisha kwa siku ambayo Guardiola hatakuweko. (Sunday Mirror)

Wakal wa mlinzi wa Manchester United Victor Lindelof, mwenye umri wa miaka 25, anasema mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Sweden alifukuziwa na Barcelona wakati wa majira ya joto. (Sport Bladet kupitia Manchester Evening News)

Uamuzi wa beki wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 19 Matthijs de Ligt kuhamia Juventus msimu huu wa joto ulitokana na hatua ya Barcelona kumfukuzia Lindelof. (Sunday Express)Matthijs de Ligt

Manchester United itaitisha £20m kwa kipa wa timu ya wachezaji wa chini ya miaka 21 wa England Dean Henderson, mwenye umri wa miaka 22, anayeichezea Sheffield United kwa mkopo, mwishoni mwa msimu. (Sun on Sunday)

Meneja wa Chelsea Frank Lampard ianaongoza jitihada za kutaka kumsajili mshambuliaji anayepigiwa upatu mwenye umri wa miaka 17 wa Wigan Joe Gelhardt. (Sunday Express)

Kocha wa Kipa wa Uhispania David de Gea, Emilio Alvarez ameondoka Manchester United baada ya kushuka kwa kiwango cha mchezaji huyo wa mwenye miaka 28 msimu uliopita, hatua iliozusha maswali kuhusu mbinu anazotumia. (Mail on Sunday)

Barcelona haina raha na mchezaji wa kiungo cha kati Arthur, mweny umri wa miaka 23, baada ya kujivinjari usiku kucha na mshambuliaji wa Paris St-Germain na raia mwenzake wa Brazil, Neymar. (Marca)

Meneja wa Juventus Maurizio Sarri ana hamu ya kumrudisha upya mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Emre Can, mwenye umri wa miaka 25, katika timu yake baada ya Mjerumani huyo kushindwa kuhamia PSG wakati wa majira ya joto. (Le10sport)

Ajax inatarajia kufikia makubaliano ya mkataba ulioimarika na mchezaji wanayemlenga wa Real Madrid, Donny van de Beek katika jitihada ya kufukuza klabu kuvutiwa na mchezaji huyo wa miaka 22 raia wa Uholanzi. (Voetbal International)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents