Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Alhamis hii, Chelsea ruksa Hazard kuondoka, Van Dijk, Pogba, Fernandes sokoni 

Chelsea wamekubali kitita cha pauni milioni 88.5 kumuuza kiungo wa kati mbelgiji Eden Hazard, 28 kwa Real Madrid.(Guardian)

Biki wa kati wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk, 27, anataka kusaini dili jingine Anfield. (ESPN)

Manchester United wako tayari kukataa ofa yeyote kwa kiungo wa kati Paul Pogba, 26. (Mail)

Wakati huohuo,United itatangaza kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na ureno Bruno Fernandes, 24,kuwa mchezaji wa kwanza kusaini kuichezea timu hiyo baada ya fainali za kombe la mataifa ulaya. (Star)

Arsenal,Manchester United na Tottenham wanamtaka mchezaji wa Stuttgart Ozan Kabak mwenye thamani ya pauni milioni 13.2 .(Express)Paul Pgba

Fenerbache wameingia kwenye kinyang’anyiro kumsajili mshambuliaji wa West Bromwich Albion Salomon Rondon.Mchezaji huyo mwenye miaka 29 anahitajika na Wolves na Newcastle,ambapo alitumia msimu uliopita (Ajansspor, in Turkish)

Southampton wamekubali kutoa dau la pauni milioni 14 kwa mchezaji wa nafasi ya ushambuliaji Standard Liege Moussa Djenepo, 20. (Daily Echo)

Kiungo wa kati Andre Gomes,25, ameonyesha nia ya kujiunga na Everton kutokea Barcelona

Inter Milan wamelenga kumsajili Kiungo wa kati wa Manchester City Taylor Richards, 18.(Sun)

Wakati huo huo, City anaamini wataipiku Chelsea kupata saini ya winga wa Millwall Samuel Edozie. (Evening Standard)FERNANDES

Norwich na Aston Villa wote wanamtolea machi beki wa kulia wa Antwerp Daniel Opare,28 ambaye atapatikana na pauni 500,000.(Sun)

Wakati huohuo, Villa wanakamilisha mipango ya kumpata mchezaji wa nafasi ya ulinzi Kortney Hause, 23, kwenda Villa Park.(Express & Star)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi Samuel Umtiti amewaambia maafisa wa klabu kuwa hana mpango wa kuondoka Barcelona majira haya, ingawa amekuwa akitolewa macho na timu za Arsenal na Manchester United. (Marca)

Juventus imemaliza mchakato wa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Sassuolo Merih Demiral, 21.kwa kitita cha pauni milioni 13 (Goal.com)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents