The Weeknd ndiye msanii maarufu zaidi duniani
Kwa mujibu wa jarida la rekodi duniani Guinness wameripoti kuwa Abel Tesfaye, anayejulikana zaidi kama The Weeknd, kitakwimu ndiye mwanamuziki maarufu zaidi kwenye sayari (the most popular musician on the planet)
Mafanikio ya mwimbaji huyo wa Canada mwenye umri wa miaka 33 yamemfanya aweke mataji mawili mapya ya rekodi ya dunia ya Guinness:
Wasikilizaji wengi wa kila mwezi kwenye Spotify – milioni 111.4 (kuanzia tarehe 20 Machi 2023)
Msanii wa kwanza kufikisha wasikilizaji milioni 100 kila mwezi kwenye Spotify
Kwa sasa The Weeknd ana karibu wasikilizaji milioni 30 zaidi kila mwezi kuliko Miley Cyrus aliyeshika nafasi ya pili (milioni 82.4).
The Weekend Pia yuko mbele ya Shakira (milioni 81.6), Ariana Grande (milioni 80.6), Taylor Swift (milioni 80.2), Rihanna (milioni 78.5), na mpinzani wake wa karibu wa kiume, Ed Sheeran (milioni 77.5).