Siasa

Mwanasiasa wa Nigeria na mke wake washtakiwa kwa kusafirisha figo

Mwanasiasa tajiri na maarufu nchini Nigeria, mke wake na “mhudumu wa afya” wamekutwa na hatia ya njama ya kusafirisha kiungo cha mwili, baada ya kumleta mwanaume wa miaka 21 nchini Uingereza kutoka Lagos.

Seneta Ike Ekweremadu mwenye umri wa miaka 60, mkewe Beatrice, mwenye miaka 56 na Dkt Obinna Obeta mwenye umri wa miaka 50, walishtakiwa kwa kula njama ya kumtoa figo mtu huyo, katika kesi ya kwanza kama hiyo chini ya sheria za kisasa za utumwa.

Ilisikia kwamba kiungo hicho kilikuwa cha binti wa wanandoa hao, Sonia, mwenye umri wa miaka 25.

Aliondolewa shtaka lile lile.

Mwathirika ambaye ni mfanyabiashara wa mitaani huko Lagos, aliletwa nchini Uingereza mwaka jana kutoa figo katika upandikizaji wa kibinafsi wa kiasi cha fedha cha £80,000 katika Hospitali ya Royal Free huko London.

Mwendesha mashtaka alisema alipewa hadi pauni 7,000 na kuahidiwa fursa nchini Uingereza kwa kusaidia, na aligundua kilichokuwa kikiendelea alipokutana na madaktari hospitalini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents