BurudaniHabari

Adidas yamuingizia Beyonce hasara, avunja mkataba

Beyoncé na Adidas wameripotiwa kukubaliana kuacha ushirikiano wao ambao ulikuwa baina ya Adidas na kampuni ya Beyonce ya mavazi  ya Ivy Park.

Chanzo kilicho karibu na mazungumzo ya biashara kilisema kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 na kampuni hiyo ambayo sana hutengeneza nguo za michezo ambayo inatoka nchini Ujerumani walifanya uamuzi wa pande zote mbili wa kusitisha ushirikiano huo, kwa mujibu wa The Hollywood Reporter.

Hitmaker huyo na Adidas walianza ushirikiano wao mnamo mwaka 2018, wakati ambapo Adidas walichukua jukumu la kutengeneza nguo za Ivy Park, wakati Beyoncé pia alifanya kazi ya viatu na nguo kwa chapa hiyo maarufu dunianni.

Habari za kuvunjwa ushirikiano huo wa kibiashara zinakuja baada ya Wall Street Journal kuripoti mnamo Februari mwaka huu kwamba kapuni ya mavazi ya Beyonce ya Ivy Park ilifanya biashara na kuingiza takriban dola milioni 40 tu ambazo ni sawa na Tsh bilioni 93.6 ikilinganishwa na matarajio ya awali ya mauzo ambayo yalitarajiwa kuwa ni $ 250 milioni ambazo nni sawa na Tsh bilioni 585 Kulingana na chanzo cha THR.

Imeelezwa kuwa pia Beyoncé na Adidas walitofautiana kuhusu tofauti za ubunifu hivi karibuni, na kusababisha kumalizika kwa mpango huo.

Mwimbaji wa Single Ladies alizindua chapa yake hiyo ya mavazi mnamo 2016, na hapo awali ilikuwa na ushirikiano na Sir Philip Green, mmiliki wa chapa ya Topshop.

Ushirikiano huo, ambao ulikuwa na mgawanyiko wa 50-50, ulikuwa wa muda mfupi, na ulivunjwa mnamo 2018 na Beyonnce alibaki na umiliki wa asilimia 100 wa Ivy Park.

Adidas bado wanaendelea kupata pigo kwenye kampuni hiyo kwa mastaa wakubwa kuacha kufanya nao kazi na hii ni baada ya Kanye West kuacha kufanya nao kazi na kuripotiwa Adidas kupata hasara kubwa.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents