HabariMichezo

Robertinho asuka kikosi cha kuimaliza Raja CA kwao

Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema maandalizi ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika ugenini dhidi ya Raja Casablanca yameanza rasmi leo.

Robertinho amesema licha ya kuwakosa baadhi ya nyota ambao wapo kwenye majukumu ya timu za taifa lakini waliopo ni wengi na programu zinaendelea kama kawaida.

Mbrazili huyo amedai kufurahishwa na uchezaji wa kikosi sababu wanazidi kuelewa mbinu zake huku akitolea mfano mechi tatu zilizopita kufanya vizuri na kupata idadi kubwa ya magoli.

“Tumeanza maandalizi ya mchezo wetu ujao dhidi ya Raja, kuna wachezaji baadhi wapo kwenye majukumu ya timu za taifa lakini waliopo tunaendeleanao na programu za mazoezi.

“Siku hizi tumebadili mfumo tunatumia washambuliaji wawili ambapo mabeki wapembeni Shomari Kapombe na Mohamed Hussein wanapanda juu kwenda kupiga krosi na mafanikio yameanza kuonekana katika mechi tatu zilizopita.”

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents