Habari

Tohara ni jambo la hiari – Dkt Kigwangalla

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto tohara ni jambo la hiari kama ilivyo matibabu mengine yote .

Dkt Kigwangalla maeyazungumza hayo leo Bungeni mjini Dodoma, wakati akijibu hoja za wabunge bungeni ambapo amesema kuwa wizara yake iliweka mikakati ya kubaini mikoa ya kipaumbele ambayo haina utamaduni wa kutahiri.

“Kwasababu tohara ni jambo la hiari kama lilivyo matibabu mengine yote ni lazima mtu atoe ridhaa yake ili aweze kufanyiwa tohara na haiwezi hata siku moja kuwa jambo la lazima na kwa mpango huo serikali haina kigugumizi kwa jambo hili lakini naomba Mhe. Spika nitoe rai kwa kina mama wote kutumia fursa ya kuwashawishi wenza wao kutafuta wakati muafaka kuzungumza na wenza wao kwa heshima na upendo wa hali ya juu wale wakina baba ambao wanashirikiana nao tendo la ndoa ambao hawajafanyiwa tohara,” amesema Dkt Kigwangalla.

“Hii itasaidia wanaume wao wenyewe kwa hiari yao kwenye vituo vinavtoa kwenye vituo vinavyotoa huduma za tohara kwasababu Mhe. Spika tohara inapunguza virusi vya Ukimwi kwa kiwango cha 60% sio kiti kidogo ni kitu kikubwa.Kwahiyo ni muhimu sana kwa wakina baba wakafanyiwa tohara na wakina mama watumie fursa watumie fursa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents