Habari

Teknolojia yabuniwa kubaini wapenzi wa jinsia moja

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Stanford nchini Marekani wameunda programu ya kompyuta ambayo inaweza kuangalia uso wa mtu na maumbile yake na kuto tofautisha kati ya wapenzi wa jinsia moja na wapenzi wengine.

Katika utafiti huo wataalamu waliunda programu kwa kutumia picha za wanaume 14,000 wazungu kutoka kwa tovuti ya kutafuta wapenzi kama alivyojitangaza katika tovuti hiyo.

Wataalamu hao wanasema programu hiyo ina uwezo wa kuwatofautisha wanaume na wanawake wapenzi wa kawaida na wapenzi wa jinsia moja kwa upande wa wanawake jaribiao hilo ilifanikiwa kwa asilimia 71. Hata hivyo programu hiyo haikufanikiwa sana, mfano wakati wa majaribio mengine walipopewa picha za wanaume mabasha 70 na wanaume 930 wapenzi wa kawaida.

Gazeti la Economist lilikuwa la kwanza kuchapisha utafiti huo na limesema kuwa miongoni mwa upungufu wa programu hiyo ni kuwam wamewatazamana zaidi wazungu na pia imetumia picha kutoka kwa mitandao ya kutafuta wapenzi.

Utafiti huo umezua mzozo mkali kati ya waliotayarisha teknolojia hiyo na watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja kusema kwamba unaweza kutumiwa kuwadhuru wapenzi wa jinsia moja.

Lakini wanasayansi wanaohusika wamesema wanaopinga programu hiyo hawajaielewa vyema mradi huo ambao utachapishwa katika jarida moja kuhusu sifa za watu na saikolojia ya kijamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents