Habari

TRA: Hakuna muda mwingine wa kuhakiki TIN number Dar

Mamlaka ya mapato chini(TRA) imesema uhakiki wa TIN number mkoa wa Dar es Salaam umekwisha na uhakiki mwingine utaendelea katika mikoa mingine.

Akizungumza na blogu ya Michuzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma ya Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo amesema uhakiki wa Tin ulikuwa ukiongezwa kulingana na mahitaji.

Mkurugenzi huyo amesema muda hautaongezwa na wenye Tin number hawatakiwi kutumia mpaka pale watakapopewa maelekezo katika ofisi za TRA ili waweze kutumia namba hizo. Hata hivyo Kayombo alisema kuwa kuwa wale wote wenye TIN namba zinazodaiwa TRA wanazo wanatakiwa kulipa kodi zao.

Uhakiki huo ulianza Agosti hadi Oktoba na kuongezwa muda tena wa miezi mitatu, uliisha jana.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents