BurudaniVideos

Tukio la maonesho ya mavazi kwa wabunifu walemavu lilivyofana (+ Video)

WAZAZI wametakiwa kutowaficha na kuwaibua wabunifu na wanamitindo wachanga wenyeulemavu ili waweze kuonyesha vipaji vyao na kujiajiri na kujipatia vipato.

Hayo yamesemwa na Mbunifu wa Mavazi nchini ambaye pia ndiye Muandaaji wa Onyesho la mavazi kwa kuinua vipaji kwa wabunifu, wanamitindo wachanga linayojulikana kama Start Tailoring Business(STB) with Augustar Masaki.

Wakati wa Onyesho hilo lililofanyika Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam, wabunifu na wanamitindo walemavu wamefanikiwa kuonyesha mavazi kwenye jukwaa hilo waliyoyashona wenyewe.

Augustar ameiambia Bongo 5 kuwa ni wakati wa kuwatoa vijana wenye ulemavu ili waweze kunufaika na vipaji vyao kwakuwa sanaa ni kazi kama kazi zingine.

“Tumeweza kufanikiwa kuwapandisha jukwaani wanamitindo 40 na wabunifu 15 wamefanikiwa kupanda kwenye jukwaa na kuonyesha mavazi waliyoyashona kwa mikono yao baada ya kupata mafunzo ya miezi mitatu.

“Nimekuwa na darasa kwa vijana wanaopenda kuwa wabunifu. Mwaka huu tumepata wenye ulemavu 10 wanamitindo na wabunifu 5 ambao wamefanikiwa kushiriki katika jukwaa hilo la mavazi,” amesema Augustar Masaki.

Aidha ameongeza kwa kuwaomba watu na makampuni kujitokeza kusaidia jukwaa hilo ili kuzidi kuwasaidia vijana na watu wenye ulemavu kuweza kujiajiri.

“Jukwaa hili nalifanya mwenyewe ninachoomba ni sapoti kutoka kwa makampuni na watu binafsi ninavyotoa mafunzo na kuandaa onyesho washindi waweze kupata zawadi kama mashine waweze kujiendeleza zaidi na kuacha kuwa omba omba barabarani.”

Pia amesema mahitaji yanayoitajika ni kama sehemu ya kufanyia onyesho machine za kunona kwa washindi, maligafi za kushonea, (vitambaa, vitenge na Khanga) ili kuzidi kufanya kazi kwa hurahisi na kuwafikia wengi wenye huitaji.

“Ni kundi ambalo linasahaulika na linahitaji msaada watakapo saidiwa kwa mara moja wataendelea na kujitafutia wenyewe kupitia ushonaji”

“Wapo wengi wenye vipaji mbalimbali kama kuchora kuimba nakucheza wakiwezeshwa wanaweza.” amesema Augustar Masaki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents