Burudani

Tunda Man adai kuhujumiwa na wasanii wenzake

Tunda Man amedai kuwa amegundua kuwepo wasanii wanaohujumu wasanii wenzao ili wasifanikiwe.

11887024_135010550185635_1531315383_n

Muimbaji huyo ameiambia 255 ya XXL kupitia Clouds FM kuwa kupitia utafiti alioufanya, amegundua wasanii hawana ushirikiano na wapo tayari kuwafanya wenzake wasifanikiwe.

“Sijakurupa kusema hivyo, nimeshafanya research na nikagundua,” alisema. “Mimi kuna siku nilikuwa na show UK, promota akaniambia natafuta namba yako kwa miaka minne, nikamuuliza ‘wewe ndio unaanza kwenye hii kazi ya upromota?’ akasema ‘hapana nimeshaleta wasanii kibao wa Bongo Flava, kila mtu nikimuuliza namba ya Tunda, wanasema hawana’, mimi nikamwambia ‘nitajie hao wanaosema namba yangu hawana’ akanitajia list ya wasanii ambao hawana namba yangu, nikagundua pia ni wanangu niko nao pia tunawasiliana. Yaani mtu ambaye nafahamiana naye na namba yangu anayo hata kwenye kichwa sio tu kwenye simu lakini anamwambia promota ‘namba ya Tunda sina’ kwa sababu anajua Tunda akija huku atapata hela nyingi,” alisema Tunda.

“Kwa upeo wangu mimi navyoona nafanya muziki tangu 2007 mpaka 2015, nina kama miaka 8 au 9. Kiukweli kabisa umoja katika Bongo Flava mimi sijauona, tunasnichian, watu hawawi real, kusnichiana ni mtu yupo radhi kukuzungumzia vibaya sehemu moja au nyingine ili apate riziki kitu ambacho kwa wenzetu mimi sikioni.”

“Kwa wenzetu mtu yupo radhi ampe dili mwenzake hata yeye kakosa, lakini sisi hapa mtu yupo radhi akuuwe na akumalize kwa promoter fulani ili mradi aje kupata yeye. Msanii mwenzako katoa wimbo mpya yaani wewe hata kushtuka, kusema jamaa kaachia wimbo mpya ngoja nimsupport! Kwa sababu kama mtu anatoa ngoma mpya wasanii wote tukamsupport tusingeona ngoma inafeli.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents