Burudani

Kim Kardashian ataja jina alilomchagulia mtoto anayetarajia kujifungua, japo hana uhakika kama Kanye atalipenda

Baada ya familia ya Kanye West na Kim Kardashian kushare na ulimwengu jinsia ya mtoto wanayetarajia kumpata siku ya Christmas kuwa ni wa kiume, sasa kinachofata ni jina.

Kim K2

Staa wa reality show ya KUWTK, Kim K (34) amesema kuwa kuna jina ambalo yeye binafsi angependa kumwita mwanaye pindi atakapozaliwa ambalo ni Easton, lakini hana uhakika kama baba yake atalipenda pia.

“Mimi nalipenda jina la Easton. Easton West. Sina uhakika kama mume wangu atalipenda hilo jina, lakini mimi nalipenda” alismea Kim.

Akizungumza kwenye ‘Ellen DeGeneres Show’, Kim alisema kuwa hajui kama Kanye pia ataliunga mkono jina hilo, lakini ana uhakika hawawezi kumpa tena jina la mwelekeo kama ‘South’ ama ‘East’ kama ilivyo kwa mtoto wao wa kwanza North West.

https://youtu.be/B8La1utC9jc

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents