Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariMakala

Uchambuzi: Ushindani wa Kibiashara kati ya Diamond na Majizzo kwenye media

Kupitia kipindi cha RECAP NA MANDO @el_mando_tz amezungumza namna @diamondplatnumz anavyozipa thamani biashara zake.

Ameanza na namna ambavyo alianza kwenye muziki na sasa amehamia kwenye media.

@el_mando_tz @diamondplatnumz amekuwa akifanya mapinduzi kwenye biashara anayoifanya.

Kwenye muziki kila mtu ameona alivyofanya hasa kwenye biashara ya kidigitali na namna anavyoipa thamani biashara yake.

Sasa akiwa kama Mkurugenzi wa media watu wanaona namna anavyotafuta vilivyobora kwenda kuipandisha biashara yake.

Mpaka sasa kwenye muziki hakuna anachodaiwa @diamondplatnumz kwa maana ameufikisha muziki sehemu ambayo ukienda kwenye mataifa mengine jina la kwanza kwenye muziki utaulizwa kuhusu @diamondplatnumz

Sasa amehamia kwenye media kuna namna ataifanya tasnia ya habari pia ithaminiwe na kuheshimika zaidi kwa namna anavyowapa heshima Watangazaji.

Watangazaji wanaopata nafasi ni wale wale na kuna haja ya kutengeneza watangazaji wapya.

Watangazaji wapya wanaoingia kwenye media kuna hana ya kukuza brand zao ili kupandisha thamani zao.

Mbali ya @diamondplatnumz kujiita Sheikh Mansour pia amepost video inayoonyesha watu wawili wakicheza Draft.

Draft linaanza kwa mtu mmoja kuanza kula kete za mwenzake lakini mwishowe aliyeanza kula kete yeye anakuja kuliwa kete zote.

Ujumbe huo unamaana kubwa sana kupitia hiki kinachoendelea kwa sasa kwenye media. – Maoni ya @el_mando_tz

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents