HabariSiasa

Uchumi wa dunia kupungua zaidi mwaka 2023

Waziri wa Fedha na Mipango , Dk Mwigulu Nchemba amesema uchumi wa dunia unatarajiwa kupungua na kufikia ukuaji wa asilimia 3.6 mwaka 2022 kutokana na uwepo wa vita kati ya nchi ya Urusi na Ukraine ambayo imesababisha kuongezeka kwa bei za vyakula na nishati hivyo, kudhoofisha zaidi matarajio ya kurejea kwa shughuli za kiuchumi zilizokuwa zimeathiriwa na UVIKO-19.

“Ikumbukwe kuwa Urusi ni nchi ya pili kwa hifadhi/uzalishaji wa bidhaa za petroli duniani ambapo inachangia wastani wa asilimia 12 katika mafuta yote yanayozalishwa dunia ikitanguliwa na Marekani yenye mchango wa asilimia 20. Aidha, Urusi ndiyo mzalishaji mkubwa wa nishati ya gesi na mafuta inayotumika katika shughuli za kiuchumi barani Ulaya,” amesema Mwigulu

Amesema kufikia mwaka 2023 na kuendelea uchumi wa dunia unatarajiwa kupungua zaidi na kufikia ukuaji wa wastani wa asilimia 3.3 kwa kipindi cha muda wa kati iwapo vita kati ya Urusi na Ukraine vitaendelea pamoja na kuendelea kuzidisha vikwazo vya kiuchumi kwa nchi ya Urusi.
#MpangowaMaendeleo2022/23
#bungelabajeti2022
#Bongo5Updates

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents