HabariSiasa

Hivi ndio vipaumbele vya Serikali kwa mwaka 2022/23

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2022/2023.

Mhe. Dkt. Mwigulu, amesema katika kutekeleza Mpango wa mwaka 2022/23, msukumo mkubwa utawekwa katika sekta za uzalishaji ambazo ni kilimo, mifugo, uvuvi na nishati kwa kuwa sekta hizi huchochea uzalishaji kwa matumizi ya ndani na mauzo nje ya nchi, hupunguza nakisi ya urari wa biashara, mfumuko wa bei na huzalisha ajira zinazowagusa wananchi wengi.

Sambamba na vipaumbele hivyo, Serikali itaendelea na utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo ikiwemo miradi ya kielelezo ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere – MW 2,115, uboreshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) pamoja na miradi ya elimu, afya, maji, usafiri wa anga na majini, bandari, maliasili na utalii, mapinduzi ya TEHAMA, miundombinu ya barabara na madaraja na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kukuza ustawi wa sekta binafsi nchini.
#Bongo5Updates
#HaliYaUchumi
#KutokaBungeni

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents