Habari

Ufaransa yatangaza masharti zaidi ya kudhibiti aina mpya ya kirusi cha Corona

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza masharti zaidi ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, wakati huu aina mpya ya maambukizi inayotwa Delta inapoendelea kusambaa kwa kasi.

Macron amesema utoaji wa chanjo utakuwa lazima kwa wahudumu wa afya, huku akitoa wito kwa raia wa nchi hiyo kwenda kupata chanjo, wakati huu serikali inapoanza kuwahamasisha watu nchini humo

Hii ni hotuba ya nane katika televisheni ya Rais Macron tangu kuzuka kwa mgogoro huu wa kiafya nchini Ufaransa. Julai 12, Emmanuel Macron alitangaza hatua mpya za kuzuia mlipuko wa nne wa aina ya kirusi kipya cha Delta kinachoambukiza haraka.

Emmanuel Macron ametangaza chanjo ya lazima kwa wauguzi na wafanyakazi wasio wauguzi katika hospitali mbalimbali, kliniki, nyumba za wazee, na pia kwa wataalamu na watu wanaojitolea kwa kuhudumia wazee.

Wahusika “wamepewa muda hadi Septemba 15 kuwa wamefanyiwa chanjo” na baada ya tarehe hii, kutafanyika “ukaguzi na vikwazo”, ameongeza katika hotuba yake kwenye runinga.

Vile vile Rais Macron p alitangaza kwamba “kampeni za chanjo” dhidi ya Covid-19 zitafanyika “tangu mwanzoni wa mwaka wa shule” kwa wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu.
By-BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents