Habari

Ujerumani yalaani walioandamana bila kuvaa barakoa

Serikali ya Ujerumani leo imelaani kile inachosema ni ukiukaji usiokubalika wa masharti ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona, baada ya maelfu ya waandamanaji wengi wakiwa bila barakoa kuandamana mjini Berlin wakipinga masharti hayo.

Thousands of Germans protest against coronavirus restrictions ...

Msemaji wa Kansela Angela Merkel Ulrike Demmer amesema waandamanaji ambao hawakuvaa barakoa au kuheshimu umbali wa mtu mmoja na mwengine wamevuka mipaka kuhusiana na haki yao ya kuandamana na kwamba kitendo hicho hakikubaliki kwa njia yoyote ile.

Demmer amesema serikali ya Ujerumani hailaani tu kukiukwa kwa masharti hayo bali jaribio la kuzuiwa kwa waandishi wa habari kuripoti kuhusu maandamano hayo na kushambuliwa kwa maafisa wa polisi. Polisi inasema maafisa wake 45 walijeruhiwa. Karibu watu 20,000 walishiriki maandamano hayo waliyoyapachika jina la ”siku ya uhuru”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents