AfyaBurudaniHabariLifestyleMichezo

Ujumbe wa Manara kwa watu wenye ulemavu wa ngozi

Ujumbe wangu kwa Rafiki zangu Wenye Ualbino.

Leo ni siku ya kimataifa ya Watu wenye Albinism Duniani,,na mimi kama Mtu mwenye Ualbino ,,naungana na Jumuiya ya Kimataifa kuwatakia kheri nyingi wenzangu wote kote ulimwenguni 🙏🏻

Najua sio rahisi kutoboa Kwa baadhi ya watu ,,hususan wenye mila potofu na imani haba hasa huku Afrika, lakini 𝗜𝗡𝗔𝗪𝗘𝗭𝗘𝗞𝗔𝗡𝗔.

Unaweza kufanya lolote lile pengine kuliko linalowezwa kufanywa na Binadamu wengine ,ikiwa una malengo sahihi, binafsi napitia changamoto nyingi za kubezwa kwa rangi yangu lakini sijawahi Kurudi nyuma.

Unaweza kuwa Msomi ,unaweza kuwa Tajiri ,unaweza kuwa Mwanasiasa ,unaweza kuwa Mwanamuziki ,unaweza kuwa Daktari ,,na hata kuwa Maarufu na Mashuhuri kweli kweli kama nilivyo mimi hii leo, licha ya Ualbino wako.

Usijisikie vibaya hata kidogo na jivunie ulivyo na mshukuru Muumba wako,ww ni sehemu ya matakwa ya Mungu aliyeahidi katika Vitabu vyake kwamba,,atawaumba Wanadaamu vile atakavyo yeye.

Endelea kutumia karama zozote alizokujaalia Mungu wako ,kuionyesha Jamii kwamba 𝗬𝗢𝗨 𝗖𝗔𝗡.

Ona kaka yako Bugati,,naishi katika kundi la Wafuasi wa Mpira wenye ushindani mwingi na baadhi yao ambao si Wastaarabu,,huja na dhihaka na matusi ya kila namna Kwa sababu mm ni Albino,,nn kinatokea? Nasonga mbele na namuangalia anaekutukana najiona nimemzidi kila kitu,,kuanzia Pesa,Jina kubwa,Umashuhuri,Wake Wazuri na hata kuishi tu maisha ya nyumbani….
anakukejeli huku ukimwangalia vema, unaweza kumuajiri kwako kupeleka Watoto shule au kusafisha Mabanda ya kuku.

Yes.. Msikubali kuwa Wanyonge hata siku moja Kwa jinsi ulivyo,,na InshaAllah Mungu atawalinda na kuwasaidia sababu yy ndio kataka iwe hivyo, na Mjivunie kwake vile alivyowaumba.

Mbarikiwe sana ndugu zangu 🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻

#Binadamuwotenisawa 👏

Related Articles

Back to top button