Burudani

Ujumbe wa Rose Ndauka kwa MC Pilipili wawachanganya mashabiki

Ujumbe wa msanii wa filamu nchini Rose Ndauka kwenda kwa MC Pilipili umezidi kujaza maswali kwa mashabiki.

12407191_274260402905678_1235728890_n

Kupitia mtandao wa Instagram, Ndauka ameweka picha ya mchekeshaji huyo na kuandika, “Mmmh haya na boo wangu nae kalala ???????????????????? sijui huwa zinanini ???????????? @mcpilipili Hongera mume wa wanawake sita…SITAKI MASWALI.”

Ujumbe huo wa Ndauka unazidi kutengeneza picha nyingi zaidi kwa mashabiki kwa kuwa hivi karibuni wawili hao wamedai kuwa na mahusiano ya kimapenzi japo hakuna aliyethibitisha hilo kati yao.

Tangu Ndauka aachane na aliyekuwa mpenzi wake Malick Bandawe aka Chiwaman ambaye amezaa naye mtoto mmoja amekuwa haweki wazi mahusiano yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents